Saturday, March 09, 2013

Rais Kikwete amjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda, Pia ahudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini Mwa Afrika nchini Afrika ya Kusini.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini jana jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).
 
 
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Freeedom Park mjini Pretoria Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyioshiriki katika harakati za ukombozi Kusini Mwa Afrika.
 
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini(Katikati) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa vyama vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika leo mchana.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa FreedomPark,Jijini Pretoria Afrika ya Kusini. Kushoto ni Rais Jakaya Kikwete mbaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni kiongozi wa ZANU PF.
 
Rais Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini ambaye pia ni kiongozi wa ANC(Watatu kushoto), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC.(picha na Freddy Maro).
 
 


No comments: