Tuesday, June 18, 2013

UTARATIBU MPYA WA KULIPIA ADA YA VISA YA KWENDA TANZANIAYAH: UTARATIBU MPYA WA KULIPIA ADA YA VISA YA KWENDA TANZANIA

Kwa wana-diaspora  wanaohitaji Visa ya Tanzania,

Tunapenda kuwaarifu kuwa kuanzia tarehe 1 Mei 2013, Ubalozi haupokei fedha taslimu wala “Credit Card” kwa malipo ya visa.
 
Malipo yote sasa yanafanyika kwenye akaunti yetu ya Benki ya NORDEA Plus Giro Na. 103 7471-8 kwa walipaji walioko Sweden. Wanaolipia nje ya Sweden watumie (BIC/Swift Address: NDEASESS na IBAN: SE2895000099604210374718 (bila kuacha nafasi).

Risiti ya malipo iambatanishwe na fomu ya maombi utakapotuma maombi kwa posta au utakapoleta maombi kwa mkono Ubalozini.

Tafadhali tunaomba ujiepushe na  usumbufu kwako   kwa kulipia ada ya visa Benki kabla ya kuleta maombi yako Ubalozini.

Taarifa hii ipo kwenye tovuti ya  Ubalozi tangu mapema mwezi Aprili kupitia “link” ifuatayo: http://www.tanemb.se//index.php?option=com_content&task=view&id=178&Itemid=36

Unakaribishwa pia kuwasiliana na Ubalozi kwa njia ya simu au barua pepe endapo utahitaji maelezo ya ziada.

Tunawaomba na tunawashauri muendelee kutembelea  mara kwa mara tovuti ya Ubalozi, www.tanemb.se ili kupata habari na taarifa mbali mbali kutoka Ubalozini.

Tunatanguliza shukrani zetu

Jacob Msekwa

KNY: BALOZI

No comments: