Sheikh Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji
yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani
kwake jijini Arusha.
Shekhe Makamba,
ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya
Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku
akiendelea na matibabu.
Akizungumza kwa
tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana
nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka
kuswali Swala ya Tarawei.
Shekhe Makamba
ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala
hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa
wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.
Alisema hata hivyo,
kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati
akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa
amesimama jirani na mlango.
Alieleza kuwa
wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu huyo akiinua mkono na
kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.
No comments:
Post a Comment