Friday, August 16, 2013

Hatimaye Mwakyembe amfunga paka kengele sakata la uvushaji madawa kupitia JNIA.


Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agnes Gerald na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Oliver Thambo nchini humo. Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara yake kuhusu suala la dawa za kulevya.
Tizama video kufahamu zaidi juu ya hatua hiiNo comments: