Monday, September 09, 2013

Tathmini ya uchaguzi mkuu Norway uliofanyika Jumatatu, 09.09.2013, Jens Stoltenberg amekubali kushindwa uchaguzi na amempongeza Bi.Erna SolbergUchaguzi mkuu hapa Norway hufanyika kila Jumatatu ya pili mwezi Septemba kila baada ya miaka minne. Jumatatu, 09.09.2013 kumefanyika uchaguzi mkuu wa Wabunge na Waziri Mkuu. 

Serikali iliyoko sasa (hadi Jumatatu, 09.09.2013) inayoongozwa na Waziri Mkuu, Jens Stoltenberg (Labour Party = Arbeiderpartiet kifupi AP) ni ya mseto kati ya AP na Socialist Left Party (Sosialistisk Venstrepartiet kifupi SV) na Agrarian Party (Senterpartiet kifupi SP) inaelekea kuwa haitaweza kurudi tena madarakani.

Mseto huo wa AP+SV+SP (unajulikana kama Red Green hapa Norway) sio kama umeshindwa hasa kouongoza nchi au sio kama umevurunda uchumi wa Norway. La hasha! Ila Wanorwejiani wamechoshwa na uongozi wa mseto huo.

Ukweli ni kuwa Tsunami ya uchumi duniani ilipotokea, Jens Stoltenberg aliiongoza Norway kwenye mstari ambao umeifanya Norway kutokuyumba yumba na kubaki moja ya nchi zilizo na idadi ndogo ya watu wasiokuwa na kazi.

Uchakavu wa serikali ya Stoltenberg umewafanya wapiga kura kutaka mabadiliko tu. Wengi ukiwauliza kwa nini wamepigia kura vyama vya upinzani? Jibu watakalokupa ni kuwa wanataka tu mabadiliko! Ukiwauliza mabadiliko yapi hayo? Hawana jibu la kuridhisha.

Inaendelea hapo juu...


No comments: