Saturday, October 26, 2013

Tunaingia majira ya theluji (Wintertime) kuamkia Jumapili, 27.Oktoba 2013Saa 9 usiku kuamkia Jumapili, 27 Oktoba 2013, hapa Norway (Skandinavia) tumebadili majira na kuingia majira ya theluji (Wintertime). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tunarudisha saa moja nyuma. 

Tuna tofauti ya masaa mawili na saa za Afrika Mashariki (East African Time = EAT) kwenye majira ya theluji. 

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 4 za asubuhi,
Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana... 

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summertime). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.


Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Wintertime). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.

No comments: