Friday, January 03, 2014


Bei ya usafiri wa Oslo na vitongoji vake kuongezeka kuanzia Februari Mosi


Kampuni ya usafiri wa mabasi na treni za mjini ya Oslo; Ruter inaongeza tiketi za usafiri kuanzia Februari Mosi, mwaka huu. Bei zitakazoongezwa ni za tiketi  za masaa 24, za siku 7, za siku 30 na za siku 365.

Bei za tiketi za masaa 24 zitaongezeka kama ifuatavyo:
Kroner 80 hadi 90 kwa watu wazima.
Kroner 40 hadi 45 kwa watoto, vijana na wastahafu.

Bei za tiketi za siku 7 kama ifuatavyo:
Kroner 220 hadi 230 kwa watu wazima.
Kroner 110 hadi 115 kwa watoto, vijana, na wastahafu.

Bei za tiketi za siku 30 kama ifuatavyo:
Kroner 630 hadi 650 kwa watu wazima.
Kroner 320 hadi 325 kwa watoto, vijana na wastahafu.
Kroner 380 hadi 390 kwa wanafunzi.

Bei za tiketi za mwaka kama ifuatavyo:
Kroner 6300 hadi 6500 kwa watu wazima.

Bei za tiketi za masaa kwa siku, hazitaongezeka

Hizo ni bei za kanda namba 1 (Zone 1). Kwa bei za zone 2, 3 na 4 angalia kiunganisho hapo chini.1 comment:

Jasa SEO said...

Great story Brother.... Nice your share ,give me alot of inspirations.thank you...