Thursday, April 17, 2014

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Othman Masoud nae aungana na UKAWA: Asema serikali TATU hazikwepekiKatika hali ya kuonyesha kuwa maoni wa wana-CCM kwenye Bunge Maalumu la Katiba, yanazidi kudhoofika kutokana na dhuluma yao kwa kufidhuli maoni na ukweli wa umma, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Othman Masoud amewaumbua wana-CCM wenzake na 201 waliobaki Bungeni kuwa serikali 3 ni ukweli uliopo wazi na ndivyo hata Katiba ya sasa inavyothibitisha, na hivyo ni ngumu sana kuufunika ukweli huo. Katiba ya sasa inazitaja wazi kuwa muungano wetu 'UNAUNDWA NA NCHI 2' na ni ngumu mno kuitaja Zanzibar bila kuonyesha nchi ya pili ni ipi, kwa hivyo serikali 3 ni jambo lililosemwa hata katika Katiba tuliyo nayo! Kauli liyowaacha CCM, midomo wazi, kimyaaa na kwa aibu kubwa hawakuthubutu kumzomea, bali wameugulia mioyo, na kuguna kichinichini! 


Chanzo:  ITV News. 

No comments: