Monday, June 30, 2014

Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) lawamani, washindwa kumchukulia hatua jambazi kutoka Nigeria linalotikisa jiji la Dar es Salaam na nchi nzima


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa; Rashid Othman.


Na Karoli Vinsent

Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service = TISS) imeingia kwenye shutuma nzito kutokana kitendo chake cha kushindwa kumthibiti, jambazi mwenye uraia wa Nigeria ambaye amekuwa akifanya uhalifu huku, jambazi huyo akijinadi kwamba hakuna wa kumchukulia hatua hapa nchini.
     
Jambazi, huyo,ambaye anajulikana kwa jina Kingsley O.Ugiagble ambae amekuwa akifanya ujambazi ndani ya nchi pamoja na kumiliki  mtambo wa kutengeneza fedha za Kimarekani “Dola” pamoja na za ndani vilevile kufanya wizi kwenye hudama za benki ATM.
  
Uchunguzi, uliofanywa na Mwandishi wa http://fullhabari.blogspot.com  huu umebaini Jambazi huyo mwenye Asili ya Nigeria ambaye anakaa maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam, kwenye nyumba ambayo yenye thamani ya shilingui milioni 250. Jambazi huyo amekuwa akihusika na mtandao wa kutenganeza fedha batili za Kimarekani yaani Dola.
    
Chanzo hicho cha habari kilizidi kusema Kingsley amekuwa anahusika kuleta silaha ambazo zimekuwa zikitumika katika vitendo vya ujambazi nchini Tanzania, huku mamlaka husika zikishindwa kumchukulia hatua.
   
Kingsley ambae amekuwa akijinadi kwamba hakuna wa kumchukulia hatua kutokana kujuana na Watendaji wakubwa ndani ya Idara nyeti ya Usalama wa Taifa, hata hivyo chanzo hicho cha habari kilimtaja jambazi huyo kuhusika kumiliki mitambo miwili ya kutengeneza fedha bandia ambayo hutumika kutengeneza noti ya shs.10000.
   
Ana mtambo mwingine unatengeneza Dola za Kimarekani ambazo sio rahisi kuzitambua.Taarifa hiyo inasema fedha hizo zipo kwenye mzunguko wa fedha kwa maana zikipitishwa kwenye utambuzi mara moja ni vigumu kuzitambua mpaka utakaporudia mara mbili ndipo  mashine hiyo utambuzi inagoma.
    
Uchunguzi wa  mwandishi wa http://fullhabari.blogspot.com  huu amebani mtambo huo wa kutengeneza fedha hizo bandia unahifadhiwa katika nyumba moja maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuendelea na mpango wake wa kudurufu fedha hizo huku Idara za Usalama wa Taifa (TISS) na zingine zinazohusika na usalama zikimwogopa jambazi huyo.
   
Kingsley, ambaye ameingia nchini kutoka nchini Nigeria bila ya pasipoti, tena wala bila hata fedha yeyote ambapo amekuwa akipata fedha nyingi kutokana na hujuma hiyo anayofanya ndani ya nchi kutokana vitendo hivyo vya kijambazi.
  
Kwa mujibu wa yyanzo vya kuamika zinasema jambazi Kingsley kabla ya kuja nchini aliwahi kufanya vitendo hivyo vya ujambazi katika nchi za Ghana, Kenya pamoja na Nigeria, ambapo hivi sasa amehamina nchini na kuendelea na vitendo hivyo.
  
Akilizungumzia hili, kigogo mmoja kutoka ndani Idara ya Usalama na ulinzi wa Taifa ambaye hakuta jina lake liandikwe mtandaoni kwa kusema yeye sio msemaji wa Idara hiyo alisema mtandao wa jambazi huyo ambae ni raia wa Nigeria ni mkubwa sana.

“Sikufichi mwandishi, huyo jambazi huyo mtandao wake ni mkubwa sana ndio maana hata sisi kumchukulia hatua tunasuasua tu, kwa sababu mara ya kwanza alikamatwa na kufika hatua ya kumrudisha kwao Nigeria lakini sisi walinzi wa Usalama kwa jjaa zetu tukazungukana nyuma tukamrejesha tena” alisema mpashaji huyo wa taarifa.
  
Duru hizo zinasema: jeuri anayoionyesha Kingsley, inatokana na kuwa na uwezo wa juu kifedha ndio maana kushindwa kuchukuliwa hatua, kwani vyombo vya habari vimekuwa vikifichua vitendo vyake huku mamlaka zikisuasua kumchukulia hatua.

No comments: