Thursday, July 10, 2014

TANGAZO MAALUMU TOKA UBALOZI WA TANZANIA; STOCKHOLM SWEDEN: KONGAMANO LA KWANZA LA DIASPORA KUFANYIKA TANZANIA TAREHE 14 HADI 15 AGOSTI, 2014
TAASISI YA TANZANIA DIASPORA INITIATIVE KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIKIANO WA KIMATAIFA PAMOJA NA OFISI YA RAIS UTAWALA BORA? ZANZIBAR NA OFISI YA WAZIRI MKUU ZIKO KATIKA MAANDALIZI YA KONGAMANO LA DIASPORA (FIRST DIASPORA HOMECOMING CONFERENCE)

KONGAMANO HILO LINATARAJIWA KUFANYIKA DAR ES SALAAM 
TAREHE 14 -15 AGOSTI, 2014 KATIKA HOTEL YA SERENA NA MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

AIDHA, KONGAMANO LITAHUSISHA PIA WIZARA, IDARA NA TAASISI ZA SERIKALI NA UMMA PAMOJA NA WAFANYABIASHARA.

KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU KONGAMANO PAMOJA NA KUJIANDIKISHA TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI HII 

www.tanzaniadiaspora.org

WATANZANIA WOTE MNAOISHI KATIKA NCHI ZA NORDIC NA BALTIC MNASISITIZWA KUSHIRIKI KATIKA KONGAMANO HILO.

UBALOZI WA TANZANIA

STOCKHOLM, SWEDEN


No comments: