Saturday, January 24, 2015

Rais Kikwete awafanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri kwa kuteua mawaziri 8Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri. Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano. Taarifa hiyo imetolewa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue. Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.

Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene

Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.

Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa

MAWAZIRI
 1. George Simachawene waziri wa nishati na madini
 2. Mary Nagu- waziri wa nchi [afisi ya rais] mahusiano na uratibu
 3. Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
 4. Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki]
 5. William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na makaazi
 6. Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na ushirika
 7. Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
 8. Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge

MANAIBU WAZIRI
 1. Stephen Masele -naibu waziri afisi ya makamu wa rais muungano
 2. Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na makaazi
 3. Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
 4. Anna Kilango naibu waziri wa elimu na mafunzo ya kiufundi
 5. Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini.

No comments: