Saturday, December 03, 2016

Tafrija siku ya Uhuru na Jamhuri, Jumamosi, 10.Desemba 2016



Mgeni wetu rasmi katika siku ya maaadhimisho ya sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika Jumamosi, tarehe 10.12.2016 katika ukumbi wa Taytu Etiopiske Restaurant, Tøyengata 2, Oslo atakuwa ni Balozi wetu wa Tanzania katika nchi za Scandinavia na zile za Baltic,
ndugu yetu mpendwa 
Balozi Dora Mmari Msechu.

Sherehe zinatarajiwa kuanza rasmi majira ya saa mbili na nusu hadi saa tisa usiku (20:30-03:00 Central European Time).

Kutakuwa na mengi na mazuri ya kushirikishana hivyo tunaombwa sana kujumuika wote kwa wingi wetu katika hili.

Karibuni nyote.

Chama cha Watanzania Oslo



No comments: