MBUNGE machachari wa Viti Maalumu (CCM),
Amina Chifupa (miaka 26),
amefariki dunia, Jumanne tarehe 26 Juni 2007
kama saa 2 na dakika 45 za usiku kwenye hospitali ya JWTZ Lugalo. Amina amefariki kutokana na ugonjwa kisukari na malaria. Mwanasiasa huyo machachari na mwenye umri mdogo kuliko wote Bungeni (ameingia Bungeni na miaka miaka 25), aliukwaa ubunge kupitia tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM.

Hakika kwake tumetoka na kwake yeye tutarudi. Mwenyeezi Mungu amsamehe madhambi yake na amjaalie Janat, (Inna Lilahi Wa Inna Ilaihi Raji'uun). Ameen!
Habari zimetumwa Jumanne, 26. Julai 2007 saa 23.55 Saa za Ulaya ya Kati:
na
Tausi Usi Ame Makame
tausi@online.no
Habari kutoka Dar es Salaam na Radio Clouds FM 22.00 News:
Radio Clouds FM ambayo Amina alikuwa mtangazaji wake kwa muda mrefu kabla ya kujitosa kwenye siasa, ilianza kupiga nyimbo za maombolezo na za dini, wakianzia wimbo wa ‘Kalale pema peponi Kamanda’, ulioimbwa na kundi la Daz Nundaz.
Ubeti wa kwanza wa wimbo huo wa Daz Nundaz unasema:
Siku mapigo yangu ya moyo yatakapokoma, Mwili utazima mfano wa nyota inapodondoka, Safari imewadia, naenda kwa Baba Muumba, Masela nawaachia ukiwa, Wambieni ndugu jamaa wapunguze kulia, Sote takwenda mbali bali ninatangulia, Dunia siyo makazi yangu tena, Niombeeni kwa Mola anilaze mahali pema, Hamtoniona tena milele, nawaachi majonzi tele, Kalale pema peponi Kamanda.”
Baada ya matangazo hayo yaliyodumu kwa takriban saa moja, ilipofika saa 4:45 usiku, mtangazaji wa redio hiyo, Gadna Habash alitangaza kwa mara ya kwanza habari za kifo hicho na baadaye kupokewa na mtangazaji mwenzake, Sebastian Ndege.

No comments:
Post a Comment