Thursday, June 28, 2007

BBC Idhaa ya Kiswahili yatimiza miaka 50


Rais Jakaya Kikwete akisalimana na bi. Flora, mjane wa hayati Oscar Kambona, mmoja wa mawaziri wa kwanza wa Tanganyika ambaye ndiye alikuwa Mtanzania wa kwanza kufanya kazi idhaa ya Kiswahili BBC London miaka 50 ilopita. JK aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya utangazji wa idhaa hiyo kwenye hoteli ya Kempinski Kilimanjaro ambapo wafanyakazi wote wa idhaa hiyo walihudhuria, aliiomba BBC pamoja na idhaa zingine za nje zinazotangaza kwa Kiswahili kutoendeleza libeneke la kutangaza mabaya tu ya bara la Afrika na kuangalia mazuri mengi yanayofanyika.

Keki ya hepibethdei ya miaka 50
ya BBC ambapo jana ilikata na kuliwa
na trupu zima la idhaa hiyo waliokuwa
Dar kusherehekea pamwe na wageni waalikwa.

___________________________

Aliisifia BBC kwa kazi nzuri na pia kueleza furaha yake kwamba Bongo ndiyo iliyofungua idhaa hiyo miaka 50 iliyopita kupitia kwa hayati Kambona na kuifanya ifikishe wasikilizaji zaidi ya 21 wakati mbongo Tido Mhando alipohitimisha jubilei yao ya dhahabu. Katika hesabu hiyo wasikilizaji milioni 13 ni wa Bongo.

Kutoka kwa: http://issamichuzi.blogspot.com/

No comments: