Sunday, July 01, 2007

Huu ni Uswahili au hulka ya binadamu?

Katika siku za karibuni kumekuwa na malamiko ya chinichini kutoka kwa mwanadada Hafsa....akilalamika kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwa msanii Banana Zorro aliyemshirikisha kwenye wimbo wake uitwao 'Presha' anafanya vitendo vinavyomuumiza hadi kufikia wakati mwingine kutoa hata machozi.

Banana Zorro (kushoto) na Hafsa (kulia)
________________________

Kwanza kabisa inasemekana wasanii hawa kwa sasa hawaongei...ingawa wenyewe wanakataa! huku kila mmoja akimshutumu mwenzake kuwa ndiye chanzo cha yote hayo

TATIZO

Hafsa anadai Banana mara nyingi akiwa mikoani...katika matangazo ya kuwaita watu kwenye show..amekuwa akiutumia wimbo huo...na hivyo wengi huudhuria wakijua kuwa yeye Hafsa atakuwepo!

Hapa anauliza kwanini Banana asitumie nyimbo zake!!!

Kingine mwanadada huyo anachosema kinamwumiza zaidi....ni kufikia mpaka Banana kumchukua dada yake mzazi kwenda nae mikoani na kaperform wimbo wa 'Presha' huku dada yake huyo akiimba sehemu iliyotakiwa kuimbwa na Hafsa.

...."wakati mwingine nafikiri anataka kunionea kwa kuwa mimi ndio kwanza nachipukia halafu ni mtoto wa kike....analalama mwanadada huyo.

......Mimi naamini tutakuja kupata mwafaka lakini pia niweke wazi kuwa sitapenda kuonewa.

".........Wimbo huu ni haki yangu na nimeusajili COSOTA,kwa hiyo kama kuna matatizo basi napaswa kupata ufumbuzi.


BANANA

Kwa upande wa Banana yeye anasema hana ugomvi na mwanadada huyo...ila vitendo vyake vya kulalamika kwenye vyombo vya habari kunamchafulia.

............."Unajua situmii wimbo huo kama anavyosema yeye,badala yake ninapokuwa naimba na bendi yangu inatokeaga watu wanauomba basi inabidi niwaimbie."

Hata hivyo Banana anapenda Hafsa atambue kwamba mashairi aliyoyaimba kwenye wimbo huo ni haki yake.

......."unajua ngoma ikivuma sana mwisho wake ni nini!Sasa hata ile tabia ya watu kuomba niwaimbie wimbo huo imepungua.Mashabiki hawapendi mambo ya malumbano.

Kutoka Dar es Salaam Hotwire.

No comments: