Tuesday, October 16, 2007

Jamani Mke Wa Mtu Sumu


Msemo huo umedhihirika baada ya mkazi wa kijiji kimoja cha nyanda za juu kusini, kuuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe, baada ya kumbamba na buzi.

Tukio hilo lilitokea baada ya mume kumtafuta mkewe na kuambiwa kuwa yuko 'natoka Dar naenda Dar' (gesti) na njemba mmoja wakijirusha kwa raha zao.

Mume huyo alimlia taimingi mkewe na kumkuta katika gesti hiyo akiagizia ulabu na hamadi!akatokea na buzi lake na jamaa alipomuuliza mkewe alikotokea akakosa majibu.

Taarifa zinasema mume halali alichomoa kisu na kumchoma kifuani mkewe mara nne na kutoa mwanya kwa buzi hilo kuchapa mwendo.


Kutoka DarHotWire.

No comments: