Saturday, October 13, 2007





Saturday,October 13, 2007 @00:03

Sir Nature atwaa tuzo ya Channel O

KIONGOZI wa kundi la muziki la Bongofleva nchini la TMK Wanaume Halisi, Juma Kassim ‘Sir Nature’ (pichani) juzi aliibuka mshindi wa tuzo za muziki zinatolewa na kituo cha televisheni cha Channel O cha Afrika Kusini.

Juma Nature aliwasili nchini jana akitokea Johannesburg Afrika Kusini alipokwenda kupokea tuzo hiyo baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha video bora ya muziki kwa wanaume kanda ya Afrika Mashariki kupitia video ya wimbo wake wa ‘Mugambo’.

Wimbo wa Mugambo uliompatia ushindi huo aliuimba alipokuwa kwenye kundi la TMK Wanaume Family kabla ya kuvunjika na kuzaa Wanaume Halisi mwishoni mwa mwaka jana.

Nature aliwania kipengele hicho cha video bora ya muziki kutoka Afrika Mashariki akichuana na nchi za Kenya na Uganda ambao ni Nameless na video ya wimbo ‘Sinzia’ , Wyre na ‘Make a Choice’ , E.A.B.C na ‘Kube', IDA na video ya Make it Hot wote kutoka Kenya pamoja na Peter Miles wa Uganda na wimbo ‘Love’.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nature kutwaa tuzo za muziki zinazotambulika kimataifa baada ya mwaka jana kushindwa kwenye tuzo za muziki za Mtv Base zilifanyika nchini Denmark.

Picha na http://watanzaniaoslo.blogspot.com

No comments: