Monday, November 19, 2007

Bila kusita tunaweza kuanza kwa kusema Lady Jaydee (pichani) ni miongoni mwa wanamuziki wa Tanzania ambao hawahitaji utambulisho mrefu sana miongoni mwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya popote walipo nchini Tanzania na duniani kote. Leo hii ukipenda waweza kumuita Jide au Lady Jaydee. Aliwahi pia kuwa na majina mengine lukuki. Unayakumbuka?

Pamoja na hayo jina lake rasmi ni Judith Daines Wambura Mbibo. Ukipenda unaweza kumuita Mrs.Gardner G.Habash jina ambalo ana haki zote za kulitumia kwani ameolewa na Gardner, mtangazaji maarufu wa Clouds FM. Judith Wambura alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 15 Juni, 1979 kwa Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Inasemekana alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujikita kwenye uanamuziki moja kwa moja mwaka 2000.

Baada ya kudumu kwa muda mrefu kama solo artist, mwaka huu Lady Jaydee amefanikiwa kufanya mambo mawili muhimu. Kwanza alianzisha rasmi bendi yake iitwayo Machozi Band na pili kutoa albamu yake ya nne aliyoipa jina Shukrani. Kabla ya hapo alishatoa albamu tatu ambazo ni Machozi (2000), Binti (2003) na Moto (2005).

Leo hii ukitaka kumuona Lady Jaydee kifanya vitu vyake akiwa na bendi yake, Machozi Band, unachotakiwa ni kujongea kila Ijumaa usiku ndani ya ZHONG HUA GARDEN, Regent Estat- Ally Hassan Mwinyi Road jijini Dar-es-salaam. Hutojutia uamuzi wako.

Hivi karibuni tulifanya mahojiano na Lady Jaydee ambapo tuliongelea mambo kadha wa kadha yakiwemo yake binafsi kama mwanandoa,binti maarufu,kazi zake za kimuziki,matarajio yake ya baadaye na mengine mengi.

Ingawa albamu yake ya Shukrani imetoka miezi kadhaa iliyopita, hatukuona haja ya kutoongelea machache juu ya albamu hiyo ambayo kama zilivyo albamu zake zilizopita, hii nayo inasambazwa na GMC Wasanii Promotors ya jijini Dar-es-salaam.Hii ndio albamu yenye wimbo uliotamba sana mwaka huu wa Siku Hazigandi (Usikilize toka kwenye YouTube...hapa kuna maneno tu). Bado inapatikana mitaani na madukani kwa wale ambao wangependa kuinunua. Yafuatayo ni mahojiano kamili;

(more…) Kutoka Bongo Celebrity


No comments: