Wednesday, November 21, 2007


Swali lililopo kwenye kichwa cha habari hii ya leo linaweza kuwa na majibu chungu mbovu. Tunaweza kuendelea kujiuliza kama tunapenda. Pamoja na hayo,jambo moja lililo wazi ni kwamba mazingaombwe ni mojawapo ya sanaa kongwe sana ulimwenguni. Kama una tafsiri yako kuhusu mazingaombwe usisite kutuambia wenzako. Tupo hapa kujifunza na kuelimishana pia.

Vilevile kama unazikumbuka enzi zile ulipokuwa shule kisha matangazo ya kuhusu ujio wa mwana-mazingaombwe yakaanza kusambaa, jamaa akaja mstarini akawapeni sample kidogo ya mazingaombwe yake,utakuwa pia unakumbuka jinsi ambavyo ulikuwa unaenda mbio ikitokea kwamba mazingaombwe yanakuja shuleni kwenu na wewe huna kiingilio. Sema ukweli, ulikuwa unafanyaje ili usiyakose mazingaombwe?

Lakini si unakumbuka kwamba kulikuwa hakuna wana-mazingaombwe wanawake? Jadi hiyo siku hizi imevunjwa na Akanashe Joan (pichani juu). Huyu inasemekana ndio mwanamke wa kwanza mwanamazingaombwe Afrika Mashariki. Sanaa hii yeye amejifunzia au kuisomea nchini China. Hivi leo ni mwanamazingaombwe maarufu nchini Tanzania akitoa burudani popote walipokusanyika watu.

Kutoka Bongo Celebrity.


No comments: