Thursday, January 24, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi A

Black Stars 1 -

Brave Warriors 0


Brave Warriors (Namibia) ilikuwa tishio kwa Black Stars.


Wachezaji wa Black Stars wakimshangilia Junior Agogo baada ya kufunga goli.

Ghana imeifunga Namibia goli moja kwa bila. Licha ya kucheza nyumbani, Ghana (Black Stars) haikucheza mchezo wa kufurahisha sana. Goli pekee la Black Stars lilifungwa na Junior Agogo, dakika ya 41 ya mchezo kipindi cha kwanza. Agogo alifunga kwa kuunganisha pasi safi toka kwa Quincy Owusu - Abeyie.


Syli Nationale 3 -

Atlas Lions 2


Guinea (Syli Nationale) wamewafunga Morocco (The Atlas Lions). Goli la kwanza la Guinea lilifungwa na Pascal Feindouno, baada ya kumzubaisha golikipa wa Morocco, Khalid Fouhami. Goli la pili la Guinea lilifungwa na Ismael Bangoura. Morocco walijipatia goli, dakika chache baada ya kufungwa goli la pili. Goli la Morocco lilifungwa na Aboucherouane. Goli la tatu la Guinea lilikuwa la penalti. Souleymane Youla aliangushwa eneo la ndani ya mita 16 na refa akaamua ipigwe penalti. Feindouno hakufanya ajiza, akafunga goli kwa ustadi mkubwa. Morocco hawakukata tamaa, walijipatia goli la pili lililofungwa na Abdeslam Ouaddo kwa kichwa.

Wachezaji wa Guinea wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Pascal Feindouno.


Ismael Bangoura akishangilia goli la pili la Guinea.


Pascal Feindouno (Kapteni wa Guinea) akifunga goli kwa penalti. Baadaye alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia rafu El-Armine Erbate wa Morocco.


No comments: