Friday, January 25, 2008


yadhamini timu 9 kati

ya timu 16 zinazocheza

fainali: Africa Cup of Nations

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma, imetiliana mkataba wa makubaliano na chama cha mpira cha Ghana (Ghana Football Association = GFA). Mkataba huo wa kuidhamini timu ya taifa ya Ghana (The Black Stars) unagharimu Dala Milioni 25 (Paundi Milioni 12.7). Puma watawapa GFA ziada ya mauzo ya vifaa vya Puma na nyongeza ya kila Black Stars itakaposhinda. Pia Puma watajenga kiwanja kipya cha mafunzo kwa timu ya taifa ya Ghana. Mkataba wa kwanza kati ya Puma na GFA unamalizika 2009. Mkataba huu mpya ni mpaka 2012.

Puma pia inadhamini timu za taifa za Misri, Angola, Kameruni, Cote d´Ivoire (Ivory Coast), Morocco, Senegal, Tunisia na Namibia.

No comments: