Sunday, January 27, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi D

Palancas Negras
(The Black Antelopes) 3



Les Lions de la Teranga
(Lions of Teranga) 1



Waaangola (Palancas Negras) wawabwaga Wasenegal (Simba wa Teranga/Lions of Teranga). Simba wa Teranga walianza kufunga goli. Lilifungwa na Abdoulaye Faye. Hadi mapumziko, Simba wa Teranga walikuwa wanaongoza kwa goli 1 - 0. Dakika 5 baada ya mapumziko, Manucho (ambaye amejiunga na Manchester United hivi karibuni) alifunga goli la kusawazisha kwa kichwa. Kwenye dakika ya 67, Manucho alifunga goli la pili baadaya purukushani kwenye goli la Simba wa Teranga. Baada ya goli hilo, Palancas Negras walitawala mchezo. Goli lililofungwa na Flavio (Palancas Negras) dakika ya 77, liliwamaliza Simba wa Teranga ambao walijitahidi kutoa makucha na meno yao makali dakika za mwisho, lakini swala weusi kutoka Angola walikuwa wajanja.

Manucho akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli la kusawazisha.


Manucho akishangiliwa baada ya kufunga goli la pili.



Les Aigles de Carthage/
The Eagles of Carthage 3


Bafana Bafana 1


Tunisia (Les Aigles de Carthage/The Eagles of Carthage/tai wa Carthage) wamewaruka juu Bafana Bafana kwa kuwafunga magoli 3 - 0. Tai wa Carthage wakiongozwa Francileudo dos Santos, Mtunisia tajinisi (naturalized Tunisian from Brazil), aliyefunga magoli 2 kati ya 3, waliwamaliza Bafana Bafana dakika za mwanzo tu za kipindi cha kwanza. Bafana Bafana wakiongozwa na kocha, Carlos Alberto Perreira, wana kazi kubwa, watakapokuwa wenyeji wa kombe la dunia 2010, kwani mchezo wa kijumla haukuwa wa kuvutia wala kuridhisha.

Thembinkosi Fanteni (Bafana Bafana) akimtoka Yassine Mikari (The Eagles of Carthage)


Hapa ilikuwa mshikemshike, Radhi Jaidi (The Eagles of Carthage) akimzuia Sibusiso Zuma (Bafana Bafana)


2 comments:

Anonymous said...

Kwa nini msitumie majina ya nchi badala ya hivyo vibwagizo? Kwa mfano, Cameroun 5, Zambia 1, halafu hizo lions na viporo zikaja baadaye. Kwa tusijua hayo majina mengine tunapata shida!

Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo said...

Tumekupata na tunashukuru kwa hilo. Tumeshafanya marekebisho kuanzia 29.01.2008

Wako,
Mhariri