Friday, January 25, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi B


The Elephants 4 -

The Squirrels 1


Timu ya taifa ya Cote d´Ivoire (Ivory Coast) au kama inavyojulikana Les Elephants (The Elephants) imeibamiza Benin (Les Ecureuils - The Squirrels au Kuchakulo kwa Kiswahili) magoli 4 - 0. Magoli ya The Elephants yalifungwa na Drogba (dakika 40), Yahya Toure (dakika ya 44), Keita (dakika ya 53) na Dindane (dakika ya 63). Goli la kufutia machozi la The Squirrels lilifungwa na Omotoyossi (dakika ya 90)


Didier Drogba (Cote d´Ivoire) akifunga goli la kwanza.


Drogba akichechemea na kutoka nje baada ya kuumia.


Super Eagles 0 -

The Eagles 0


Kwenye mechi ingine kwenye kundi hili, Super Eagle (Nigeria) wametoka sare na The Eagles (Mali). Nafasi ya The Super Eagles kuendelea kwenye robo fainali ni finyu. Wanapaswa kuwafunga Benin, ili kuwa na matumaini ya kuingia robo fainali.


Seyi Olafinjana (Nigeria) akipiga shuti huku Mahamadou Diarra (Mali) akifanya jitihada kumzuia


Dramana Traore (na. 10 wa Mali) akimtoka mchezaji wa The Super Eagles


Frederic Kanoute (Mali) akimtoka John Obi Mikel (Nigeria)

No comments: