Saturday, January 26, 2008

Kigogo' akamatwa na kiganja

cha mkono kilichokaushwa.


Na Mwandishi Wetu, Tabora

Polisi mkoa wa Tabora imewatia mbaroni watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na risasi tano na kiganja cha mkono wa binadamu kilichokaushwa nyumbani kwa mwanakiji mmoja Minguya, kata ya Upuge Mkoani Tabora....

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Muhidin Mshihiri watu hao waliokamatwa Jumatatu iliyopita walitajwa kuwa ni Shaban Mussa mkazi wa Isoke wilayani Urambo, Peter Dilongo na Dilongo Luka, wakazi wa Ninguya wilayani humo.

Kamanda Mshihiri alisema kuwa watu hao walikamatwa nyumbani kwa Shabani Ali Kasiga mkazi wa Ninguya ambapo walikuta nje ya nyumba yake risasi tatu za smg na moja ya G2b na bunduki aina ya shortgun na kiganja cha mkono wa binadamu kilichokaushwa.

Habari zilisema kuwa risasi hizo pamoja kiungo hicho cha binadamu vilikutwa vimefichwa na watuhumiwa hao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ugomvi wa mipaka ya shamba.

Watu mbalimbali wa eneo hilo walikuwepo wakati watuhumiwa hao wakikamatwa walidai kuwa mtuhumiwa mmoja kati ya hao Peter Dilongo ni kigogo wa eneo hilo.

“Huyu kigogo amekamatwa? Alihoji mwananchi mmoja aliyekuwepo eneo hilo ambaye jina lake halikuweza kufahamika.

Kutoka Global Publishers TZ.

No comments: