Sulley Muntari wa Black Star anaichezea timu ya Portsmouth ya Uingereza
Black Star yaanza vizuri.
Timu ya taifa ya Ghana "Black Star" jana ilianza vizuri kwenye fainali za kombe la mataifa ya Afrika "Africa Cup of Nations" baadaya ya kuifunga Guinea kwa magoli 2 - 1.
Mechi ilianza saa 17.00 za Afrika Magharibi kwenye uwanja wa Ohene Djan mjini Accra. Kipindi cha kwanza kilipomalizika matokeo yalikuwa 0 - 0
saa 18:16
Goli la kwanza la Black Star lilifungwa kwa penalti na Asamoah Gyan baada ya Junior Agogo kuangushwa kwa rafu na Oumar Kalabane wa Guinea. Kipa wa Guinea, Kemoko Kamara alishindwa kuchukua shuti kali la Asamoah.
saa 18.25
Guinea walipata kona. Kona ilipigwa na Pascal Feindouno na Oumar Kalabane akasawazisha kwa kichwa.
saa 18.50
Sulley Muntari aliipatia Black Star goli la ushindi baada ya kupiga kiki kali toka kama yadi 30 hivi.

No comments:
Post a Comment