Vigogo wa Usalama wachunguza taarifa BoT |
Na Mwandishi Wetu
UCHAMBUZI wa taarifa ya ukaguzi wa Benki Kuu Tanzania (BoT) kuhusu upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Kigeni (EPA) umeanza.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilisema wananchi wengi wamejitokeza kutoa taarifa zinazoendelea kuisadia timu iliyoundwa kufanya kazi hiyo.
Ili kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika kwa uhakika na kikamilifu zaidi, timu hiyo iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufanya kazi hiyo imetoa namba za simu za wajumbe wake, ili kuwarahisishia wananchi kuendelea kutoa taarifa.
Wajumbe na namba zilizotolewa kwenye mabano ni
* Inspekta Jenerali wa Polisi, Bw. Said Mwema (0754 785557)
* Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
Bw. Robert Manumba (0754 206326).
* Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea
(0754 763741)
* Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,
Bibi Lilian Mashaka (0754 336116).
Taarifa hiyo iliwahakikishia wananchi wote, kwamba taarifa watakazotoa zitakuwa msaada mkubwa kwa timu na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali ambayo inafanyiwa kazi.
"Kila mwananchi atakayetoa taarifa, atapata hifadhi ya faragha kwa mujibu wa sheria," ilisema taarifa hiyo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni MWenyekiti wa Timu hiyo.
No comments:
Post a Comment