Wednesday, January 23, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi D


Mamadou Niang wa Senegal "Teranga Lions" (jezi ya kijani) akigombania mpira na Jaidi wa Tunisia (jezi nyeupe)


Francileudo dos Santos (Mtunisia mwenye asili ya Brazil) akikabiliwa vizuri na Moustapha Sall wa Senegal.


Teranga Lions 2

The Carthage Eagles 2

Goli la dakika za mwisho lililofungwa na Isaam Jooma liliiwezesha Tunisia (The Carthage Eagles) kutoka sare 2 - 2 na Senegal (Teranga Lions). Tunisia ndiyo iliyokuwa ya kwanza kujipatia goli dakika ya 9 lililofungwa na Issam Jomaa. Goli la kusawazisha la Senegal lilifungwa na Moustapha sall. Senegal walipata goli la pili, lililofungwa na Diomansy Kamara.


Mchezaji wa Palancas Negras (jezi nyekundu) akigombani mpira na mchezaji wa Bafana Bafana.

Palancas Negras 1

Bafana Bafana 1.

Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Angola (Palancas Negras) wametoka suluhu na Afrika Kusini (Bafana Bafana) kwa kufungana goli moja kwa moja. Goli la Angola, lilifungwa na Manucho baada ya kupokea pasi toka kwa Flavio. Goli la kusawazisha la Bafana Bafana lilifungwa na Elrio van Heerden dakika za mwisho za mechi.

Andre (Angola, jezi nyekundu) akiangaliwa kwa makini na Teko Modise wa Bafana Bafana.


No comments: