Robo fainali
Ghana 2
Nigeria 1
Nigeria 1
Ghana (The Black Stars) wameingia nusu fainali baada ya kuwatoa wapinzani wao wa jadi Nigeria (The Super Eagles). Nigeria ndio walikuwa wa kwanza kufunga. Goli la Nigeria lilifungwa na Yakubu dakika ya 34 kwa penalti. Ghana wakicheza nyumbani, walijitahidi sana, na jitihada zao zilizaa matunda kwenye dakika ya nyongeza (47), baada ya Michael Essien kufunga goli la kusawazisha kwa kichwa.
Baada ya mapumziko, kila timu ilianza kwa uangalifu. Baada ya muda mambo yakaanza kuchanganyika. Kapteni wa The Black Stars, John Mensah alipewa kadi nyekundu, baada ya kumfanyia rafu Odemwingie wa Nigeria. Baada ya Mensah kutolewa Ghana ilifanya mabadailiko ya kimchezo (walibadili na kucheza 4-4-1), Michael Essien alirudi kuwa beki, Sulley Muntari alirudi na kuwa kiungo katikati, wakamwacha Junior Agogo pekee yake kama mshambulizi.
Goli la ushindi la Ghana lilifungwa na Junior Agogo akiwa pekee mbele ya goli dakika ya 82 ya mchezo baada ya kupokea pasi safii toka kwa Sulley Muntari.
No comments:
Post a Comment