Tuesday, February 05, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Robo fainali

Kameruni 3

Tunisia 2

baada ya dakika 120.


Shabiki wa Kameruni, jana Jumatatu 4.2.2008


Kameruni wakishangilia goli lilifungwa na Geremi, jana Jumatatu 4.2.2008


Tunisia wakishangilia goli lililofungwa na Chouki Ben Saada, jana Jumatatu 4.2.2008


Kameruni (Lions Indomptables/ Indomitable Lions) imeingia kwenye nusu fainali baada ya kuwafunga Tunisia (Les Aigles de Carthage/The Eagles of Carthage). Baada ya dakika 90 za mchezo timu zilikuwa 2 - 2. Ikabidi zichezwe dakika 30 za nyongeza na ndipo Stephane Mbia wa Kameruni alipofunga bao la 3 la ushindi kwa Kameruni. Magoli ya Kameruni yalifungwa na Mbia (dakika ya 19), Geremi (27) na Mbia (92). Yale ya Tunisia yalifungwa na Chouki Ben Saada (35) na Chikhaoui (81).


Nusu fainali, Alhamisi 7.2.2008

Ghana vs. Kameruni

Ivory Coast vs. Misri


No comments: