Robo fainali
Misri 2
Angola 1
Angola 1
Penalti iliyopigwa na Hosny Abd Rabou na goli lililofungwa na Amr Zaki yameiwezesha mabingwa wa Africa Cup of Nations 2006, Misri (The Pharaohs) kuingia nusu fainali. Goli la kwanza la Misri lilipatikana baada ya Andre Macanga (Angola = Palancas Negras/The Black Antelopes) kuunawa mpira golini kwake baada ya "frikiki". Manucho (Angola) alisawazisha dakika ya 27. Kijana mchezaji mpira mzuri, hii inaonyesha jinsi Sir Alex Ferguson (Kocha wa Manchester United) alivyokubali kumsaini msimu huu. Licha ya kuwa Angola (Palancas Negras/The Black Antelopes) kutolewa kwenye fainali za mwaka huu, wameonyesha kuwa ni timu ya kutia matumaini kwenye fainali za 2010 zitakazofanyika nchini kwao Angola.
Timu zilianza hivi:
Egypt: 1-Essam Al Hadari; 5-Shady Mohamed, 6-Hani Said, 20-Wael Gomaa, 14-Sayed Moawad; 8-Hosni Abd Rabou, 11-Mohamed Shawky, 7-Ahmed Fathi, 22-Mohamed Aboutrika; 10-Emad Moteab, 19-Amr Zaki.
Angola: 1-Lama; 2-Marco Airosa, 5-Kali, 6-Yamba Asha, 15-Rui Marques; 8-Andre, 10-Maurito, 11-Gilberto, 17-Ze Kalanga; 16-Flavio, 23-Manucho
No comments:
Post a Comment