Saturday, February 09, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Nafasi ya tatu yashikwa na Ghana


Ghana 4

Ivory Coast 2



Suley Muntari alipiga shuti kali toka yadi 25 na kufunga goli la kwanza la Ghana dakika ya 10 ya mchezo. Boubakar Sanogo (Ivory Coast) alisawazisha dakika ya 24. Dakika ya 32 Ivory Coast walipata goli lililofungwa na Sanogo. Baada ya Ivory Coast kupata goli la pili walianza kutawala mchezo, kwa kipindi cha dakika kadhaa hivi walionekana kama wangeshinda mechi hii. Zikiwa zimebakia dakika 20 mpira kwisha, Quincy Owusu - Abeyie alisawazisha kwa wenyeji wa fainali, Ghana. Junior Agogo alifunga goli la tatu, baada ya kupokea pasi safi toka kwa Michael Essien. Goli la nne la Ghana lilifungwa na Haminu Draman dakika ya 85. Ghana wamekuwa washindi wa tatu kwenye fainali hizi.


Timu zilikuwa hivi:

Ghana:
Kingson, Sarpei, Pantsil, Mensah, Addo (Barusso 90), Annan, Essien, Muntari, Draman (Afful 89), Agogo, Baffour (Quincy 20). Marizevu: Adjei, Gyan, Kingston, Asamoah, Ayew, Kumordzi, Dauda, Asare, Alhassan.


Waliofunga magoli:
Muntari 10, Quincy 70, Agogo 80, Draman 85.


Ivory Coast:
Tiassa Kone, Boka, Zoro, Fae (Dindane 83), Romaric, Tiene, Zokora, Sanogo, Kalou (Gervinho 73), Drogba, Keita (Toure Yaya 64). Marizevu: Barry, Toure, Gohouri, Arouna Kone, Meite, Bakari Kone, Loboue, Djakpa, Eboue.


Magoli yalifungwa na:
Sanogo 24, 32.


Refarii:
Jerome Damon (Afrika Kusini).



Michael Essien (Ghana) na kipa wa Ivory Coast Tiasse Kone wakiangalia shuti kali la Suley Muntari likitinga wavuni. Lilikuwa goli la kwanza la Ghana.

Wachezaji wa Ivory Coast wakipongezana walipopata goli la kwanza.


Didier Droga (Ivory Coast) akimtoka mchezaji wa Ghana


Junior Agogo (Ghana) akiwajaribu kuwatoka walinzi wa Ivory Coast, Didier Zokora (nam. 5) na Arthur Boka (nam. 3)


No comments: