Saturday, February 09, 2008

Kona ya Jumamosi


Sifiki ”mwisho wa safari”


Anti Dina Saturday Feb 09, 2008

Swali:

ANTI mimi ni msichana wa miaka 24, tatizo langu ni kwamba huwa nasikia wenzangu wakihadithia wanavyofika mwisho wa safari zao, lakini kwangu mimi jambo hilo sijaliona, yaani sijawahi kufika mwisho wa safari yangu kwenye makasheshe, nini kinasababisha?

B.M.K

Jibu:

Kushindwa kufika mwisho wa safari kwa kitaalamu tatizo hili huitwa (anorgasmia) linaweza kusababishwa na mambo kadhaa. Mambo ya saikolojia na maumbile yanahusika katika jambo hili. Kushindwa kusisimka au kuandaliwa vizuri ni moja ya sababu, lakini pia mkandamizo wa mawazo, msongo wa mawazo, na matatizo ya uhusiano yanaweza kuwa sababu ya kukufanya wewe ushindwe kufikia mwisho wa safari yako.

Sababu nyingine ni za kiafya, mkandamizo wa mawazo ya kila siku pengine kutokana na hali ya maisha hukufanya kushindwa kuiweka akili yako katika makasheshe na hivyo kupoteza uwezo wa kufikia mwisho wa safari. Hata hivyo, tatizo hili hutibika kirahisi kwa wengi wanaokumbwa nalo, kuna makala na vitabu vingi vimeelezea kwa undani namna ya kuondokana na tatizo hilo na njia nyingine ni kuondokana na mambo niliyoeleza hapo juu.

Pia, kuna tiba zinazotolewa hospitalini na ushauri kutoka kwa wataalamu bingwa wa magonjwa
ya wanawake na wanasaikolojia. Kuna vidonge kama vya Prelox, ‘krimu’ aina inayojulikana kwa jina la ‘Vibrance - TC, vidonge vya Prozac, Zoloft, Paxil, Haldol , Thorazine na Mellaril vinatibu tatizo hili na utafikia mwisho wa safari kwa raha zote.

Sababu nyingine ya kutofikia mwisho wa safari ni maradhi yanayoshambulia sehemu za uzazi na kusababisha kushindwa kufikia mwisho wa safari.


No comments: