Sunday, February 10, 2008

Africa Cup of Nations 2008


Mabingwa ni Misri

kwa mara ya sita



Misri 1

Kameruni 0



Misri au Egpyt (The Pharaohs) wamenyakua ubingwa wa mataifa ya Afrika mwaka huu baada ya kuwafungwa Kameruni goli 1 kwa bila. Goli hilo lilipatikana dakika ya 77 ya mchezo, baada ya Mohamed Zidan kumzidi nguvu mlinzi mkongwe wa Kameruni, Rigobert Song na kumpa pasi Mohamed Aboutrika aliyekuwa pekee na golikipa wa Kameruni, kameni na kufunga goli. Baada ya Kameruni kufungwa waliamka na kuanza kushambulia goli la Wamisri. Wamisri wakicheza kwa ushrikiano kama sisimizi, walikuwa wagumu kutoa mwanya....


Timu zilikuwa hivi:

Kameruni: Kameni, Tchato, Song, Atouba, Emana (Idrissou 56), Song Billong (Binya 16), Mbia, Epalle (M'Bami 65), Geremi, Nkong, Eto'o. Marizevu: Hamidou, Mbarga, Angbwa, Essola, Makoun, N'Guemo, Tomou, Job.

Waliopewa kadi za njano: Atouba (Kameruni), Idrissou (Kameruni).

Misri: El Hadari, Mohamed, Hany Said, Gomaa, Moawad, Fathi, Hassan, Abd Rabou, Aboutriaka (Ibrahim Said 89), Moteab (Zidan 60), Zaki (Shawky 84). Marizevu: Abdel Monssef, Sobhy, El Saeed, Fathallah, Gamal, Mostafa, Shaaban, El Mohamady, Fadl.

Aliyepewa kadi ya njano: Hassan.

Goli lilifungwa na: Aboutrika dakika ya 77.

Refarii: Coffi Codja (Benin)

Watazamaji: 35,500

Fainali za mashindano haya zitafanyika Angola 2010


Mashabiki wa Misri


Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Aboutrika akizuiwa na Stephanie Mbia (Kameruni)


Golikipa, Essam El - Hadari anapaswa kusifiwa kwa
kuiwezesha Misri kuwa mabingwa 2008

Mohamed Abourtika, mfungaji wa goli pekee kwenye fainali.




No comments: