Makundi ya vijana Kenya sasa yawageukia wanawake wavaa suruali |
NAIROBI, Kenya
HALI ya machafuko nchini imezidi kuchukua sura mpya baada ya kutoka katika siasa na kuingia katika ukabila sasa hali hiyo imebadilika tena na kuingia katika jinsia. Hali hiyo ya kijinsia imekuja baada ya kundi la vijana kupiga marufuku wanawake wote kuvaa suruali kwa kile wanachodai mwanamke wa kiafrika hapaswi kuvaa suruali zaidi ya sketi na gauni.
Tukio hili lilitokea jana katika mji wa Naivasha baada ya kundi la vijana kuanza kuwasakama wanawake wote waliokuwa wamevalia suruali na kuwalazimisha wazivue huku likitangaza kuwa litahakikisha wanawake wanavaa sketi na magauni tu. Katika kituo cha mabasi cha mjini Naivasha wanawake ambao walikuwa wamevalia suruali walijikuta katika hali ngumu baada ya kundi hilo la vijana kuwalazimisha washuke kwenye matatu na kuwaamuru kuwa hadi wavae vizuri ndio waendelee na safari zao.
Mmoja wa wanawake ambaye alikumbwa na dhahama hiyo, Miriam Wairimu ameelezea jinsi alivyonusurika kuvuliwa nguo hizo hadharani baada ya kundi hilo kumteremsha kwenye matatu huku likimlazimisha avue nguo hiyo. Nililazimishwa kushuka kwenye matatu na nilikuwa sijafika mjini kwa muda wa wiki moja iliyopita ndio nikakutana na kundi hilo la vijana likinilazimisha kwamba nivue suruali, alisema Miriam ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha kompyuta katika mji huo.
Mwanamke wa kiafrika hapaswi kuvaa suruali na tunaka kuhakikisha jambo hilo linabaki hivyo hivyo hapa Naivasha, alisema mmoja wa vijana katika kundi hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe. Nilitimua mbio huku kundi hilo likinifukuza hadi nilipookolewa na mama moja ambaye alinipatia sketi katika duka la kushona nguo, aliongeza dada huyo. Amelalamika kwamba hali hiyo ni ya unyanyasaji kwa mwanamke.
Nilitimua mbio huku kundi hilo likinifukuza hadi nilipookolewa na mama moja ambaye alinipatia sketi katika duka la kushona nguo, aliongeza dada huyo. Amelalamika kwamba hali hiyo ni ya unyanyasaji kwa mwanamke.
No comments:
Post a Comment