wenyewe kwa wenyewe
Ushirikiano baina ya wasanii wa kike umekuwa ni hafifu sana. Maneno haya yanazungumzwa na wengi sana hapa nchini. Inakuaje wasanii wa kike hawapendani wenyewe kwa wenyewe? Inawezekana ni wivu unaowasumbua au kila mmoja anajiona bora kuliko mwenzake?
Habari hii imefanyiwa uchunguzi wa kina na timu nzima ya Dar411 na kubainika ya kwamba ni ukweli kabisa kwamba kuna sababu maalumu zinazowafanya wasanii wa kike nchini wasiwe kitu kimoja lakini habari hizi hazikuweza kutambulika zaidi.
Kuna sababu ya kwamba kila mtu anajiona bora kuliko mwenzake na hivyo kumsikilizia mwenzake. Inawezekana wazi ya kwamba hakuna anayemvutia pozi mwenzake lakini. Mdau mmoja wa muziki wa nyumbani anayetambulika kwa jina la Safina Kassanga aliidhibitishia Dar411 ya kwamba alishawahi kuwaona wasanii fulani wa kike wakiliana pozi laivu na wakapishana bila ya hata salamu bila ya sababu yeyote.
Mdau huyu kwa maoni yake na timu ya dar411 alisema ni wivu tu unaowasumbua wanamuziki wa kike kwani kila mmoja anajiona bora kuliko mwenzake. Naye mwanamuziki wa kutoka kundi la Wakali Kwanza, Makamua alisema ya kwamba yeye haelewi kwanini wasanii wa kike hawana ushirikiano kama walivyo wao, ila ameshashuhudia wasanii wa kike wakiliana mikausho. Msomaji wa safu hii, je unaweza ukasema ni kwanini wasanii wa kike nchini wana chuki za wenyewe kwa wenyewe bila sababu malumu?
Sifikirii kuwa na mume sasa
Huyu si mwingine bali ni Hawa, mwanamitindo anayeipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini China. Ni msichana mrembo na mwenye haiba yenye mvuto. Dar411 iliweza kumbamba mrembo huyu na kuweza kuzungumza naye machache.
Hawa alichonga na Dar411 na kusema tangu awasili nchini kwa likizo yake amekuwa akisumbuliwa sana na wanaume na ahadi kemkem bila kujua lengo lake kuu ambalo la kutotaka kusikia neno kuolewa. Mwanamitindo huyu alisema amekuwa akitumia muda wake mwingi kwenye masuala ya umodo hivyo kuweka mambo ya mapenzi benchi kwakuwa muda wake bado haujamruhusu kuwa mke wa mtu.
"Sifikirii kuolewa siku za karibuni kwakuwa fani yangu hairuhusu kabisa mtu aliyeolewa kabisa, na kwa upande wangu naona ni sahihi kabisa kuolewa wakati huu ambao nang'aa kwenye fani hii. Mwanamitindo huyu ametokea mkoa wa Dodoma kwenye familia ya wasichana wanne na shoo yake ya kwanza kufanya catwalk ilikuwa ni Golden Tulip na baada ya hapo alipata mkataba wa kufanya kazi huko nchini China ambapo mpaka sasa anafanya kazi zake nchini humo.
Kutoka Dar 411
No comments:
Post a Comment