Miss Tanzania abambwa akijiuza...
Na Issa Mnally
Mmoja kati ya washiriki wa Fainali za Miss Tanzania mwaka jana (jina tunalo) na ambaye alifanikiwa kutinga hatua ya 10 bora, katika shindano hilo, lililochukua nafasi kwenye Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, amebambwa akijiuza.....
Mrembo huyo, alinaswa na waandishi wa gazeti hili, kwenye eneo linaloizunguka Corner Bar, iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kumpiga picha kadhaa.
Awali, gazeti hili, lilitonywa na chanzo chetu kuwa mrembo huyo amekuwa akijiuza kwa wanaume ili kujipatia pesa za kujikimu na hali ngumu ya kimaisha, baada ya Miss Tanzania kushindwa kumpa mafanikio aliyokuwa akiyahitaji.
Chanzo hicho, kilifafanua: “Hafanyi siri na eneo lake ni pale pale Corner Bar, akifika mapema huwa anakaa ndani ya baa kama mteja wa kawaida, lakini kwa wanaomjua, huwa wanambeba kama ‘kawa’, ingawa ni kwa bei mbaya kidogo.
“Ikifika ‘night kali’ (usiku wa manane) hapo huwa anajiachia bila wasiwasi, anajichanganya na ‘machangu’ wengine barabarani na kutafuta wateja. Wakati huo hata wale wenye chenchi ndogondogo wakimbambatiza wanambeba.”
Baada ya kupata udaku huo, gazeti hili, liliingia ‘chimbo’, kumwinda mrembo huyo, kabla ya usiku wa manane wa kuamkia jana, kumnasa akiwa katikati ya ‘msitu’ wa machangudoa wenzake, huku akivuta sigara.
Hata hivyo, baada ya kubaini kuwa analengwa na kamera zetu, mrembo huyo alijificha katikati ya warembo wenzake.
Aidha, baada ya kupata upenyo, Miss Tanzania huyo alikimbia, lakini mpigapicha wetu, aliyekuwa kwenye gari, alimfungia kazi na kumkimbiza, ambapo alifanikiwa kumpiga picha chache kwa nyuma.
Zoezi hilo, lilikuwa ni eksheni namba moja kwa mwaka 2008, bado Ijumaa Wikienda lipo kazini, likimfuatilia mrembo huyo. Kama hatojirekebisha, basi katika siku zijazo, tutamtaja jina na kuichapisha picha yake halisi.
No comments:
Post a Comment