Sunday, June 29, 2008

Elizabet Joseph:

Kutoka ukahaba

hadi ushauri nasaha


Angela Semaya.

MSEMO ‘mtoto wa mwenzio ni wako, mlinde’ una lengo la kuikumbushia jamii umuhimu wa kuthamini watoto. Lakini pia kwa mtu mmojammoja kufahamu kuwa ana wajibu wa kumlinda mtoto ye yote hata kama si wake.

Kwa mtazamo wangu kama kila mmoja katika jamii angethamini mtoto wa mwanzake huenda tusingesikia habari za mikasa ya kutisha, matukio ya udhalilishaji na unyanyasaji wa watoto kama yaliyomtokea Elizabeth Joseph.

Kama isingekuwa mwanamke mmoja kutoka kijijini kwao kumtorosha na kumleta katika Jiji la Dar es Salaam, Elizabeth, binti huyo wa miaka 25 pengine asingeteseka, kubakwa, kuingia katika biashara ya ukahaba, kutumia dawa za kulevya na mwisho kujikuta akiwa ni muathirika wa virusi za Ukimwi.


Bofya na endelea>>>>>



No comments: