Sunday, June 29, 2008


España, campeona

de Europa

Hispania 1 = Ujerumani 0



Kocha wa Hispania, Luis Aragonés


Senna akimdhibiti Schweinsteiger


Torres akimvisha nusu kanzu golikipa wa Ujerumani Jens Lehmann na kufunga goli


Torres akinyonya kidole baada ya kufunga goli


Torres akiwapungua mkono mashabiki wa Hispania

Casillas akishangilia ushindi


kapteni na kipa wa Hispania Iker Casillas akinyanua kombe. Picha kutoka Getty Images, Reuters na AFP.

Hatimaye Hispania mabingwa wa mataifa ya Ulaya, baada ya miaka 44! Mara ya mwisho Hispania kunyakua kombe hilo ilikuwa mjini Madrid mwaka 1964.

Hispania walianza kwa uangalifu kwa kucheza pasi fupi fupi. Ujerumani ikajibu mapigo na dakika 10 za kwanza, Ujerumani walionekana kama wangetawala mchezo. Hispania wakaamka wakaanza kucheza kwa uhakika. Pasi zao zilikuwa za kiustadi kama daktari mpasuaji (surgical precision). Dakika ya 33 ya mchezo, Senna alitoa pasi kwa Xavi alitoa pasi ya kupima kwa rula, Torres akaipokea na kumpita Philipp Lahm na akamvisha nusu kanzu kipa wa Ujerumani Jens Lehmann na kufunga goli pekee na la ushindi kwa Hispania. Kipindi cha pili kilianza kama kilivyoanza kipindi cha kwanza, kwa Ujerumani kuanza kuutawala uwanja, lakini Hispania wakautawala mchezo dakika zote zilizobaki.

Timu zilikuwa kama zifuatazo:

Hispania:

Iker Casillas (kipa na kapteni), Carlos Marchena, Carles Puyol, Andrés Iniesta, Xavi Hernández, Fernando Torres (alitolewa dakika 78), Cesc Fàbregas (alitoka dakika ya 63), Joan Capdevila, Sergio Ramos, Marcos Senna, David Silva, Marizevu: Andrés Palop, Pepe Reina, Raúl Albiol, Fernando Navarro, David Villa (alitoka dakika ya 66), Santi Cazorla (aliingia badala ya Villa), Xabi Alonso (aliingia badala ya Fabregas), Sergio García, Daniel Güiza (aliingia baada ya Torres kutoka), Álvaro Arbeloa, Juanito, Rubén de la Red na kocha: Luis Aragonés.

Ujerumani:

Jens Lehmann (kipa), Arne Friedrich, Bastian Schweinsteiger, Torsten Frings, Miroslav Klose (alitolewa dakika ya 79), Michael Ballack (kapteni), Thomas Hitzlsperger (alitolewa dakika ya 58), Philipp Lahm (alitolewa dakika ya 46), Per Mertesacker, Lukas Podolski, Christoph Metzelder, Marizevu: Robert Enke, René Adler, Marcell Jansen (aliingia badala ya Lahm), Clemens Fritz, Heiko Westermann, Simon Rolfes, Mario Gómez (aliingia badala ya Klose), Oliver Neuville, Piotr Trochowski, Tim Borowski, David Odonkor, Kevin Kuranyi (aliingia badala ya Hitzlsperger) na kocha: Joachim Löw

Refarii alikuwa Roberto Rosetti kutoka Italia.

Mechi lilichezwa kwenye uwanja wa Ernst Happel mjini Vienna.



1 comment:

Anonymous said...

Haya wenzetu hata Kihispania mnakijua sisi wengine tulie tu..