Monday, June 09, 2008



Jana kwenye fainali za nchi za Ulaya (Euro 2008) kundi B, Kroatia imeifunga wenyeji wa fainali Austria kwa goli 1 - 0. Goli la Kroatia lilifungwa kwa penalti na Luca Modric.

Mechi ingine kwenye kundi B Ujerumani ilibamiza Poland kwa magoli 2 - 0. Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Lukas Podolski kwenye dakika ya 20 na 72. Podolski alikataa kushangilia magoli aliyofungwa kwa vile moyo wake bado uko Poland, lakini kwa vile ni mashindano na ni Mjerumani sasa alibidi afunge magoli! Kwenye timu ya Ujerumani, wachezaji wawili wana asili ya Poland nao ni Lukas Podolski na Miroslav Klose. Podolski alizaliwa kwenye mji wa Gliwice na Klose alizaliwa Opole.

Leo kuna kivumbi kwenye kundi C (kundi la kifo) Ufaransa inachuana na Romania na Italia inachuana na Uholanzi. Kama Uholanzi itaifunga Italia, basi itakuwa ushindi wao wa kwanza kwa miaka 30. Mara ya mwisho Uholanzi kuifunga Italia ilikuwa 1978 (magoli 2 - 1) kwenye Kombe la Dunia nchini Argentina.

No comments: