Monday, June 09, 2008

Maalim Seif:

Nipo tayari kukamatwa


na Saada Said, Zanzibar

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutosita kumkamata iwapo inataka kufanya hivyo.

Alisema iwapo serikali inataka kumkamata yeye yupo tayari, kwani ameshazoea kukamatwa na hilo halitamzuia kuwatetea wananchi wanyonge kwa kuwa ni mtetezi wao licha ya vitisho vya muda mrefu anavyovipata.

“Endeleeni kunichunguza, si afadhali huko kunichunguza kuna makubwa zaidi ya hayo ambayo yameandaliwa kwangu mimi na wenzangu…. hawa wameshazoea, madhalimu wakubwa, hakuna serikali yenye kufanya udhalimu kama hii, waje kunikamata,” alisema katibu mkuu huyo.


Bofya na endelea>>>>>

No comments: