Tuesday, June 17, 2008


Kundi C

Uholanzi Romania 2 – 0

Uholanzi ikiwa tayari washindi wa kundi hili ilipumzisha baadhi ya wachezaji wake, kama kipa Edwin van der Sar, Giovanni van Bronckhorst, Ruud van Nistelrooy, Wesley Sneijder, Nigel de Jong Ilipata goli la kwanza lililofungwa na na Huntelaar kwenye dakika y 54. Van Persie aliwamaliza Waromania kwenye dakika ya 87 kwa kufunga goli safiii sanaaa!!


kipa wa Romania Bogdan Lobonţ` akimwamia refarii awe makini

Ibrahim Afellay akitmtoka Adrian Mutu wa Romania


Orlando Engelaar mfungaji wa goli la kwanza la Uholanzi



Italia Ufaransa 2 – 0

Italia ikijua kuwa kutoa droo na Ufaransa na Uholanzi kufungwa na Romania ndio mwisho wao kwenye fainali hizi, ilicheza kwa juhudi zao zote. Mafanikio yao yalianza kuonekana kwenye dakika ya 24 baada ya Abidal (benki wa Ufaransa) kumwangusha Luca Toni ndani ya mita 16. Pirlo alifunga goli kwa penalti. Goli la pili la Italia lilifungwa na De Rossi kwenye dakika ya 61.


Eric Abidal akimkata mkwanja Luca Toni na kusababisha penalti na kupewa kadi nyekundu


Thiery Henry baada ya kugusa "free kick" iliyomgusa na kuwa goli ya pili la Italia


Kijana mpenzi wa Ufaransa akiwa kwenye mshangao!


Mpenzi wa Italia akiwa na furaha ya kuingia robo fainali

No comments: