Sunday, June 15, 2008


Kundi D

Hispania 2 = Sweden 1

Hispania imeonyesha nia yake ya kuwa mabingwa wa Ulaya baada ya kuwafunga Sweden. Goli la kwanza la Hispania lilifungwa na Fernando Torres (dakika ya 15). Sweden walisawazisha dakika ya 34 kwa goli la Zlatan Ibrahimovich. Sweden walionyesha kupwaya baada ya Zlatan kutoka kwa sababu ya maumivu ya misuli yanayomsumbua hata kabla ya fainali hizi.


David Villa baada ya kufunga goli la ushindi kwa hispania dakika ya 92.


Wachezaji wa Sweden baada ya Zlatan Ibrahimovich kusawazisha


Fernando Torres (nam. 9) akifunga goli la kwanza la Hispania



Ugiriki yavuliwa ubingwa

Urusi 1 = Ugiriki 0

Warusi wamewavua Ugiriki ubingwa na kuwatoa kwenye fainali za mataifa ya Ulaya. Antonis Nikopolidis golikipa wa Ugiriki alifanya kosa la kijinga, akanyang´anywa mpira na Sergej Semak akampa pasi Konstantin Zyrjanov aliyefunga goli la pekee na la ushindi kwenye dakika ya 32. Nafasi ya kwanza kwenye kundi hili imechukuliwa na Hispania ikiwa na pointi 6, huku Sweden na Urusi zikiwa na pointi 3 kila moja. Mechi ya mwisho kwenye kundi hili itakuwa baina ya Hispania na Ugiriki / Sweden na Urusi. Sweden au Urusi lazima mmoja wao ashinde. Zikitoka sare hakutakuwa na dakika za nyongeza, zitapigwa penalti baada ya dakika 90.


Antonis Nikopolidis akifanya kosa la kijinga na Sergej Semak akamnynganya mpira na kutoa pasi kwa Konstantin Zyrjanov aliyefunga goli

Konstantin Zyrjanov akifunga goli la pekee la ushindi la Urusi



No comments: