Kombe la dunia 2010

Dar es Salaam
Picha na Muhidin Issa Michuzi.
Timu ya taifa (Taifa Stars) ikiwa kwenye kinyang´anyiro cha kuwania kucheza fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini 2010, jana imetoka suluhu (0 – 0) na Kameruni (Indomitable Lions) kwenye uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam.

Mchezaji nyota wa Timu ya Taifa ya Cameroon na Klabu ya Barcelona ya Hispania, Samuel Eto’o, usiku wa kuamkia juzi alionyesha tabia mbaya (ufuska) baada ya kutoroka kambini usiku na kuonekana akijivinjari na mrembo wa Kitanzania. Mchezaji huyo wa kutegemewa ambaye pamoja na wenzake walifikia kambini katika Hoteli ya New Africa ya jijini Dar es Salaam, hakuweza kufahamika alitoroka saa ngapi lakini alibambwa saa 6 usiku katika Hoteli ya Golden Tulip ‘akitanua’ na kimwana huyo ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja...
Bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment