Thursday, June 19, 2008

Mbunge wa CCM:

Nchi imeuzwa



na Martin Malera

MJADALA wa hotuba ya bajeti ya 2008/09 unazidi kuchukua sura mpya kila siku, huku wabunge wakiendelea kutoa kauli kali dhidi ya serikali.

Katika hatua ambayo inaweza kushtua, Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu, naye ameungana na watu wanaoikosoa wazi wazi serikali kwa kusema kuwa viongozi wameiuza nchi bila sababu na hivi sasa wananchi wana hasira dhidi ya viongozi hao.

Nyarandu alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa hotuba hiyo ya bajeti.


Bofya na endelea>>>>>

No comments: