Nimchome nisimchome!
Na Richard Bukos
‘Nimchome nisimchome’ Hivi ndivyo inavyoweza kutafsiriwa ishara inayoonekana kutolewa na shabiki mmoja wa Bendi ya Msondo Music ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja (pichani mbele) alipokuwa akisakata muziki na mnenguaji wa bendi hiyo, Nacho Saidi, ‘Mama Nzawisa’ huku akiwa amevaa viatu vyenye ncha kali (mchongoko) na kuwaduwaza mashabiki....
Shabiki huyo ambaye ilibainika kuwa ni daktari bingwa wa watoto wa hospitali moja ya jijijini Dar es Salaam, alikuwa akiselebuka na mnengeuaji huyo katika Ukumbi wa Africentre, jijini mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu, mnenguaji wa bendi hiyo alikuwa akinengua jukwaani kwa kuzungusha kiuno chake kama pia ndipo daktari huyo aliyekuwa akipata kinywaji alishindwa kuvumilia na kuinuka kitini kwenda kuvamia jukwaa hilo kwa madaha ya hali ya juu.
Baada ya kuvamia jukwaa, daktari huyo aliyekuwa amevaa viatu vya mchongoko na pamba za bei mbaya, alionyesha ubingwa wa hali ya juu katika kusakata msondo na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu zote.
Wakati daktari huyo akiendelea na vituko vyake, dada mmoja aliyekuwa akishuhudia vituko hivyo ambaye alionesha kumtambua daktari huyo alisikika akimwambia mwenzake;
“Jamani huyu baba ni daktari bingwa, kuna kipindi mwanangu alikuwa akisumbuliwa na maradhi fulani ni yeye ndiye aliyemuokoa, du!!! kumbe akichangamka hufanya mambo ya uhakika,” alisema dada huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana.
Kutoka Global Publishers (T)

No comments:
Post a Comment