”Operesheni Benin”
machangudoa 58 na
makuwadi 18 kutoka
Naijeria wakamatwa
Kina dada wa Kinaijeria wakiwa wamejipanga kusubiri wateja kwenye mitaa ya Skippe, Dronning, Banken na maeneo kuzunguka Benki Kuu mjini Oslo. Alfajiri kuamkia jana polisi walivamia "apartments" mjini Oslo. Hapa ni mojawapo kwenye mtaa wa Trondheim. Picha kutoka Dagbladet
Kuamkia jana alfajiri, mapolisi 100 wa Oslo walishiriki kwenye ”Operesheni Benin” na kuwakamata machangudoa kutoka Nigeria na makuwadi wao, Wanorweji wenye asili ya Nigeria. Makuwadi 18 na machangudoa 58 wamekamwata. Hao makuwadi 18 kazi yao ilikuwa ni kuwatafutia tiketi wasichana toka Nigeria na kuwaleta Norway, kuwapatia sehemu za kuishi ili waje kufanya shughuli za uchangudoa. Faida kubwa iliyokuwa ikipatikana ilikuwa inachukuliwa na makuwadi hao, kiasi kidogo ndicho walichokuwa wanaachiwa hao wasichana. Kumekuwa na ongezeko kubwa la wasichana kutoka Nigeria kuja kufanya shughuli hizo hapa Norway. Kivutio kikubwa ni hela wanazopata kwa mteja mmoja ni kubwa kuliko sehemu zingine za Ulaya.
Wakazi wengi wa Oslo wamekuwa wakilalamika kwa kuparamiwa na hao kina dada kutoka Nigeria kwenye mtaa maarufu mjini Oslo uitwao Karl Johan nyakati za jioni na usiku. Kutokana na wingi wao, wameshusha bei ya huduma zao kwa kiwango cha chini sana kiasi cha kuwaharibia shughuli machangudoa wa Kinorweji.
Wengi wa wasichana hao wana vibali vya kuishi na kufanya kazi kutoka nchi zingine za makubaliano ya Schengen, hivyo basi wana uhuru wa kufanya shughuli hizo hapa Norway. Biashara ya ukahaba haijapigwa marufuku, ila muswada uko Bungeni na punde si punde itakuwa haramu kwa wateja kununua huduma zinazotolewa na hao machangudoa.
Vyanzo vya habari zetu vinatuelezea kuwa miongoni mwa makuwadi waliokamatwa ni baadhi ya wenye asili ya Naijeria tunaowafahamu. Dada mmoja kati ya hao alikuwa amepanga ”apartments” 10 kila apartment alikuwa analipa kroner 7000 hadi 10000 halafu anazipangisha kwa machangudoa kwa kroner 12000 hadi 13000,- kwa mwezi. Huyo dada hafanyi kazi lakini gari analoendesha ni la kroner milioni moja na nusu na safari za Dubai hazimwishi. Dada mwingine anamiliki duka la vipodozi na vyakula vya Kiafrika mjini Oslo.
Mwingine ni jamaa mmoja ambaye amewahi kwenda Makka kuhiji. Yeye na mkewe wamekamatwa.
1 comment:
Bora polisi wameamua kuchukua hatua hizo. Dada zetu wanatutia aibu. Hata sisi tukipita Karl Johan usiku tunaonekana kama machangudoa. Tukienda kwenye madisco tunakataliwa kuingia kwa kuhisiwa kama machangudoa......
tausi@online.no
Post a Comment