Thursday, June 19, 2008

Robo fainali

Ujerumani Ureno 3 – 2


Ujerumani ikicheza kwa kushambulia na kujilinda timu nzima, imeweza kuzima makali ya Christiano Ronaldo/Ureno. Ujerumani walianza kwa kuwabana Wareno na kuwasumbua kiasi cha kuwafanya wasicheze kama walivyozoea. Goli la Ujerumani lilikuwa kama ukuta wa Berlin (kama ya 1989) Schweinsteiger alifungua goli la Ureno kwenye dakika ya 22. Dakika ya 26 Miroslav Klose aliongeza goli la pili kwa Ujerumani.

Ureno walipata goli kwenye dakika ya 40 baada ya Ronaldo kuwatoka walinzi wawili wa Ujerumani na kupiga shuti kali, lakini Lehmann akapangua kwa mguu na Nuno Gomes akapata nafasi ya kufunga. Michael Ballack alifunga goli la tatu kwa kichwa baada ya kumsukuma beki wa Ureno Paulo Ferreira (mchezaji mwenzake Chelsea). Ilikuwa na faulo ya wazi lakini refarii aliifungia macho. Dakika za mwisho Ureno walifanya mashambulizi makali kwenye goli la Ujerumani na walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kwenye dakika ya 86 lililofungwa na Postiga. Ujerumani inaingia nusu fainali.

Robo fainali ya kesho ni kali ya Uturuki na Kroatia



Joao Mautinho (Ureo) akishangaa baada ya kukosa goli

Ronaldo akimtoka Philipp Lahm beki wa Ujerumani


Bastian Schweinsteiger akifunga goli

No comments: