Slaa afichua siri
ya EPA
Dr. Willbrod Slaa
KAMBI ya upinzani bungeni, imepinga kauli iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo kuwa fedha zilizochotwa katika akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) si za serikali bali za wafanyabiashara ambao baadhi yao hawapo hivi sasa.
Akitoa hotuba ya kambi ya upinzani kujibu Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma jana, Dk. Willibrod Slaa alisema fedha hizo ni mali ya Watanzania ambazo zimetokana na Programu iitwayo ‘Debt Buy Back Program’ na si za wafanyabishara walizolipa kwa ajili ya kununua bidhaa nje kama alivyosema Waziri Mkulo.
Alisema ukaguzi mbalimbali uliofanywa na kampuni za ukaguzi zilithibitisha kuwa kampuni 22 zilifanya biashara na kampuni hewa na hakuna mfanyabiashara aliyeweka fedha.
No comments:
Post a Comment