Monday, June 16, 2008


Uturuki yafanya

maajabu!

ilikuwa nyuma kwa

magoli 2 kwa sifuri

hadi dakika ya 75

yashinda magoli 3 – 2

Mechi hii ni moja ya mechi zilizosisimua wapenzi wa soka kwenye fainali hizi. Mpaka dakika ya 75 Chekia ilikuwa inaongoza kwa magoli 2 kwa sifuri. Magoli ya Chekia yalifungwa na Koller (dak. 34) na Plasil (dak. 62). Uturuki hawakukata tamaa hata kidogo. Wakilishambulia goli la Chekia kama nyuki, Uturuki walipata goli la kwanza dakika ya 75 lililofungwa na Arda. Goli la kusawazisha lilifungwa na Nihat (dak. 87). Golikipa wa Chekia, Petr Cech alifanya makosa makubwa na mpira ukamponyoka, Nihat akasema ”Alhamdullilah” na kusawazisha na alifunga goli la ushindi dakika ya 89. Uturuki wanacheza na Kroatia kwenye robo fainali


Jan Koller akishangilia goli alilofunga


Kapteni Nihat Kahveci (Uturuki) baada ya kufunga goli la pili


Nihat Kahveci & Arda Turan (Turkey)


Uswisi yaaga fainali

kwa heshima na

taadhima

yaifunga Ureno 2 – 0

Licha ya kuwa tayari wameshayaaga fainali za mataifa ya Ulaya, Uswisi walicheza kwa bidii na kuifunga Ureno kwa magoli 2 – 0. Magoli ya Uswisi yalifungwa na
Hakan Yakin (dakika 71, 83).

Hakan Yakin (Uswisi) akipongezwa na kocha wake baada ya kufunga goli la kwanza


Hakan Yakin akifunga goli la pili



No comments: