Thursday, June 12, 2008

Watanzania wamjia juu

swahiba wa Kikwete


WATANZANIA kadhaa wamejitokeza na kumshutumu rafiki wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni mwekezaji katika sekta ya madini, James Sinclair, kwa kuanika hadharani kwa wawekezaji wenzake, ripoti ya Kamati ya Rais ya Madini ambayo bado ni siri.

Wananchi kadhaa wamekuwa wakipiga simu katika ofisi za gazeti hili na kueleza kushangazwa kwao na hatua ya Bw. Sinclair kuweka hadharani yale yaliyomo katika ripoti hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais Kikwete kukabidhiwa ripoti hiyo.



JAMES Sinclair

Gazeti hili liliripoti katika moja ya safu zake, toleo lililopita, kwamba Bw. Sinclair ameandika waraka na kuuweka katika tovuti ya kampuni yake akiwaeleza wawekezaji wenzake katika sekta ya madini Tanzania kwamba amefanikiwa kuisoma ripoti hiyo ambayo bado ni ya siri, na kwamba ina mambo ambayo ni ya manufaa kwao.


Bofya na endelea>>>>>

Soma barua ya wazi kwa Sinclair toka Jamiiforums


4 comments:

Anonymous said...

Sinclair anajiamini kiasui hicho kwa sababu yuko karibu sana na Rais Kikwete. Hell no...huu jamaa anaweza kuwa jasusi wa Kanada

http://en.wikipedia.org/wiki/Canadian_Security_Intelligence_Service

http://en.wikipedia.org/wiki/Communications_Security_Establishment

Kwa jinsi alivyo karibu na viongozi wetu na jinsi habari za nchi zinavyovuja kama tunavyosikia, jamaa akizipata anazirusha kwao!!! Who knows!!!

Sijui Tanzania Intelligence and Security Service wako makini na hilo? Au kama wasemavyo Wazamo:

"kalaga baho!"

Anonymous said...

Mwacheni Sinclair amwage radhi si bure katumwa huyo,na pia alizipataje si wamempa makusudi. Habari zenyewe hata uyo raisi akizotoa hadharani hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa dhidi ya mafisadi hao, hasa ya nini subira.

Anonymous said...

Ni ya serikali kama ingekuwa kuzivujisha hizo habari si wangezitoa kwenye baadhi ya magazeti kuliko kumpa mgeni? Huku serikali zikitaka kuzivujisha habari "siri" wanazitoa kwenye vyombo vya habari na si kwa wageni. Huyo aliyempa Sinclair hizo habari ni msaliti wa Tanzania!!!!

Anonymous said...

Ni = Nia